Watoto watano katika jimbo la Texas
nchini Marekani waliokutana na mwanamume
anayeugua Ebola nchini humo,
wanachunguzwa kwa karibu nyumbani kubaini ikiwa wana dalili zozote za
ugonjwa huo.Kwenye mkutano na wandishi wa habari katika hospitali ya Texas Health Presbyterian mjini Dallas, gavana wa jimbo hilo alisema kuwa wazazi wa watoto hao wana wasiwasi lakini aliwahakikishia kuwa hakuna tisho la maambukizi.
Mgonjwa huyo Thomas Duncan anaaminika kuambukizwa Ebola alipokuwa nchini Liberia.
Bwana Duncan yuko katika hali mbaya kwa mujibu wa wahudum,u wa afya wanamuhudumia.
Alimwambia kuwa alikuwa ametembelea Liberia, lakini taarifa aliyokuwa anatoa hakuwa ameitoa kwa kikosi kizima kilichohusika na matibabu yake hospitalini.