Mtandao wa Facebook umewaomba radhi
jamii ya wanaume na wanawake waliobadili jinsia yao au (transgender) kwa
kusisitiza kuwa lazima watumie majina yao halisi kwenye
kurasa sao za
mtandao huo.Kurasa nyingi za watu wa jamii hiyo zilianikwa au kufichuliwa na mtumiaji mmoja mwezi jana kwa kutumia majina bandia.
Akaunti hizo, zilisemekana kuwa bandia kwa sababu wamiliki wake walikuwa wametumia majina yasio yao kama vile, Lil Miss, Hot Mess, badala ya kutumia majina yao halisi kama vile, Bob Smith kwenye kurasa zao.
''Nataka kuwaomba radhi wale wote waliohisi kutendewa ubaya kutokana na sakata hii.Hii ni kwa sababu Facebook inataka watu watumie majina yao halisi wala sio utambulisho bandia.'' Hata hivyo
Watu hao walikuwa wametishia kuondoka kwenye mtandao huo na kuandaa maandamano makubwa mjini San Francisco.
Msemaji wa watu wa jamii hiyo,Mark Snyder, alisema wameridhika baada ya Facebook kuwaomba radhi.
Alisema kuwa sio watu wa jamii hiyo pekee wanaotaka kutumia majina ambayo sio yao ili kujilinda kutokana na kejeli kwenye mitandao.
Hata hivyo Facebook imekuwa ikisisitiza kuwa watumiaji wa Facebook sharti watumie majina yao halisi ili wapeukane na kejeli kwenye mtandao pamoja na watu kutumia majina yao.