MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa,
Freeman Mbowe amewateua
Dk. Willbrod Slaa kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara
na Salum Mwalim ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Viongozi hao
wameteuliwa jana usiku na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema hivyo
kufikia tamati ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.Mhe. John Mnyika
anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Mbunge wa Jimbo
la Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe ambaye aliondolewa katika nafasi
hiyo na kamati kuu ya chama hicho kwa kudaiwa kuvunja katiba ya chama.