
Kwa Mujibu wa Admiral Kirby, kuuawa kwa Godane ni pigo kubwa zaidi kwa kundi hilo la Al shabaab na itasaidia kukabiliana na ugaidi unaofanywa na kundi hilo eneo la Afrika Mashariki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na washirika wake wakuu kukabili wapiganaji hao wa AL shabaab ambapo katika miaka ya hivi karibuni wamezidisha mashambulio sio tu nchini Somalia bali hadi nchi jirani.
Wiki iliyopita Kikosi cha kulinda amani chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika AMISOM kikishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia kilianzisha oparesheni kali kuwasaka wapiganaji hao wa AL shabaab. Na kufikia mwanzoni mwa wiki hii Marekani ikajiunga katika oparesheni hiyo ambapo walishambulia msafara ambao Ahmed Godane alishukiwa kuwa nda